Sunday, April 21, 2013

BADO KUNA KAZI KUBWA YA KUFANYA - DI CANIO.

MENEJA wa klabu ya Sunderland Paolo Di Canio amefanikiwa kuibadilisha timu hiyo kuwa moto wa kuotea mbali katika wiki tatu ambazo ametwaa madaraka lakini mwenyewe amedai kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha wanabakia katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Sunderland ambao ushindi waliopata wa mabao 3-0 dhidi ya mahasimu wao Newcastle mwishoni mwa wiki iliyopita na mwingine wa bao 1-0 dhidi ya Everton umeipaisha timu hiyo kwa alama sita toka katika mstari kwa kushuka daraja. Wakiwa wamebakiwa na mechi nne kabla ya ligi kumalizika Sunderland wanaonekana wako katika nafasi nzuri ya kubakia kwenye ligi kuu kwa msimu wa saba mfululizo lakini Di Canio hadhani kama juhudi hizo zinatosha ili kubakia huko. Kwasasa muda kusheherekea bado kwani bado kuna kazi ya kufanya na kama wakifanikiwa kushinda mechi yao dhidi ya Aston Villa hapo wanaweza kuwa na uhakika wa kutoshuka daraja msimu huu.

No comments:

Post a Comment