Sunday, April 21, 2013

HOENESS AKIRI KUCHUNGUZWA KWA KUKWEPA KODI.

RAIS wa klabu wa Bayern Munich ya Ujerumani, Uli Hoeness amebainisha kuwa anachunguzwa kama amewahi kukwepa kodi na Mamlaka ya Kodi ya nchi hiyo. Hoeness ambaye ni nyota wa zamani wa Ujerumani Magharibi alikataa kuongelea kwa undani zaidi suala hilo lakini alikiri kuwa na akaunti katika benki nchini Switzwerland. Hoeness alikaririwa akisema kuwa binafsi tayari aliomba taarifa za akaunti yake kutoka kwa muhasibu wake januari mwaka huu lakini hakuona kama kuna tatizo lolote la kimahesabu na kuahidi kutoa ushirikiano kwa maofisa hao wa kodi mpaka watakapomaliza shughuli zao. Kwasasa Hoeness amedai kuwa anasubiri kwa hamu mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona ambao utachezwa Jumanne usiku katika uwanja wa Allianz Arena.

No comments:

Post a Comment