Monday, April 22, 2013

TAJI LA 20 MAN UNITED LANUKIA.

Ligi kuu ya soka nchini England itaendelea tena leo kwa mchezo mmoja kati ya Manchester United watakaokuwa nyumbani kwenye uwanja wa Old Traford kuwakaribisha Aston Villa. Mchezo huo ambao Manchester United inahitaji ipate ushindi kujihakikisha ubingwa wa 20 wa ligi kuu soka nchini England na kuweka rekodi mpya ya kuwa timu iliyochukua taji hilo mara nyingi zaidi ya Liverpool ambayo ilikuwa inashikilia rekodi ya mataji 19. United inakwenda kwenye mchezo huo ikiwa imetoka kulazimishwa sare ya 2-2 na West Ham United katika mchezo wa jumatano iliyopita wakati Aston Villa wao watashuka uwanjani kucheza mchezo huo usiku wa leo wakiwa kwenye harakati za kuepuka kushuka daraja la ligi kuu. United katika michezo mitano iliyopita waliyocheza wamefungwa michezo miwili,wameshinda miwili na kutoka sare mmoja huku Aston Villa katika michezo mitano iliyopita waliyocheza wamefungwa mchezo mmoja na kushinda michezo mitatu na kutoka sare moja dhidi ya Fulham. Huu utakuwa mchezo wa 34 kwa timu zote kwenye ligi kuu soka nchini Uingereza msimu huu ambapo zitakuwa zimebakisha michezo mingine minne kumaliza ligi.

No comments:

Post a Comment