Monday, April 22, 2013

DROGBA, ETO'O WATAJWA KUGOMBEA TUZO YA GOLDEN FOOT.

MANAHODHA wa timu za taifa za Ivory Coast na Cameroon, Didier Drogba na Samuel Eto’o wameteuliwa katika orodha ya wachezaji tisa watakaogombania tuzo ya Golden Foot ambayo kwasasa inashikiliwa na Zlatan Ibrahimovic aliyenyakuwa mwaka jana. Drogba na Eto’o ndio wachezaji pekee kati ya tisa ambao ni waafrika katika tuzo hiyo ya kimataifa ambayo hutolewa kwa wachezaji kutokana na mafanikio yao waliyopata kwenye soka. Wengine walioteuliwa ni pamoja na David Trezequet wa Ufaransa, Miroslav Klose wa Ujerumani, Andrea Pirlo wa Italia, Andres Iniesta na Iker Casillas wote kutoka Hispania na Frank Lampard na David Beckham wa Uingereza. Tuzo za Golden Foot hutolewa kwa wachezaji waliofikisha umri wa miaka 29 na mshindi hawezi kushindania tena tuzo hiyo. Waliowahi kushinda tuzo hizo kipindi cha nyuma ji pamoja na Roberto Baggio (Italia, Brescia) 2004: Pavel Nedved (Jamhuri ya Czech, Juventus) 2005: Andryi Shevchenko (Ukraine, AC Milan) 2006: Ronaldo (Brazil, Real Madrid) 2007: Wengine Alessandro Del Piero (Italia, Juventus) 2008: Roberto Carlos da Silva (Brazil, Fenerbahçe) 2009: Ronaldinho (Brazil, AC Milan) 2010: Francesco Totti (Italia, Roma) 2011: Ryan Giggs (Wales, Manchester United) 2012: Zlatan Ibrahimovic (Sweden, PSG)

No comments:

Post a Comment