Monday, April 15, 2013

MBIO ZA UBINGWA WA LANGALANGA BADO ZIKO WAZI.

DEREVA nyota wa langalanga kutoka timu ya Ferrari, Fernando Alonso amesema mbio za ubingwa wa dunia wa mashindano hayo msimu huu bado ziko wazi. Kauli ya dereva huyo imekuja baada ya kufanikiwa kushinda mbio za China Grand Prix ambazo ni za kwanza kushinda kwa msimu huu wa 2013. Ushindi huo unamuweka Alonso ambaye ni raia wa Hispania katika nafasi ya tatu nyuma ya dereva wa Red Bull Sebastian Vettel anayeongoza na Kimi Raikkonen wa Lotus anayeshika nafasi ya pili katika msimamo wa orodha hizo. Alonso amesema kwasasa anadhani Ferrari, Lotus, Red Bull na Marcedes wote wana nafasi ya kufanya vizuri msimu huu ndio maana ni mapema sana kutabiri atakayetawadhwa bingwa msimu huu. Dereva huyo aliendelea kusema kuwa kama wataendelea kuwa katika nafasi za juu mpaka katika kipindi cha mapumziko ya kiangazi watakuwa wamejiweka katika nafasi nzuri ya kunyakuwa taji la dunia.

No comments:

Post a Comment