Monday, April 15, 2013

DI CANIO AMZAWADIA MAMA YAKE USHINDI WAKE WA KWANZA SUNDERLAND.

MENEJA wa klabu ya Sunderland ya Uingereza, Paolo Di Canio amemzawadia ushindi wa timu yake iliyopata kwa mara kwanza chini yake, mama yake aliyefariki dunia mwaka mmoja uliopita. Katika mchezo huo Sunderland walifanikiwa kuwafunga mahasimu wao Newcastle United kwa mabao 3-0 na kufufu a matumaini ya klabu hiyo ambayo iko katika hatari ya kushuka daraja. Di Canio ambaye saa 24 kabla ya mchezo huo alikuwa katika misa ya maadhimisho ya mwaka mmoja wa kifo cha mama yake, amesema kuwa kabla ya kuanza kwa mchezo huo aliona sura ya mama yake ikimjia kichwani ndio maana ameamua kumzawadia ushindi huo muhimu. Furaha haikuwa kwa Di Canio peke yake kwani pia mashabiki wa klabu hiyo walionyeshwa kufurahishwa na ushindi huo wa kwanza mnono wakiwa ugenini kwa mahasimu wao hao baada ya kupita miaka zaidi ya 34.

No comments:

Post a Comment