Monday, April 15, 2013

MASHABIKI WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI BRAZIL.

VYOMBO vya habari nchini Brazil vimerioti kuwa mashabiki wawili wa soka nchini humo wamepigwa risasi na kufa wakati wakielekea katika Uwanja wa Castelao Arena uliopo katika mji wa Fortaleza. Kwa mujibu wa taarifa hizo mashabiki hao walikuwa wakielekea kuishangilia timu ya Ceara ambayo ilikuwa ikicheza na wenyeji Fortaleza kabla ya vijana hao kuanzisha vurugu kwa kuwarushia mawe wapinzani wao ambao nao walijibu mapigo na kupelekea vifi vyao. Taarifa hizo ziliendelea kudai kuwa tukio hilo lilitokea maeneo ya karibu na uwanja huo ambao ni mojawapo ya viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2014. Katika mchezo huo ambao ulizua tafrani hiyo Ceara walifanikiwa kuwafunga mahasimu wao Fertaleza kwa bao 1-0.

No comments:

Post a Comment