Monday, April 15, 2013

NEYMAR ATAKUWA MBADALA WA MESSI BARCELONA - CURY.

MWAKILISHI kutoka Brazil, Andre Cury ambaye anashughulikia masuala mengi ya klabu ya Barcelona katika ukanda wa Amerika Kusini anaamini kuwa kusajiliwa kwa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Brazil na timu hiyo itamaliza tatizo la kumtegemea Lionel Messi. Mengi yameongelewa kuhusu umuhimu wa nyota huyo wa kimataifa wa Argentina katika kikosi cha Barcelona na Cury anadhani Neymar ambaye anacheza katika klabu ya Santos atakuwa mbadala wa Messi katika safu ya ushambuliaji. Cury amesema Barcelona inamhitaji Neymar ndio maana imemuweka katika orodha ya juu kati ya wachezaji ambao itawasajili na watakuwa tayari kuanza mazungumzo pindi nyota huyo atakapoamua kuondoka Brazil. Aliendelea kusema kama Neymar akihamia Barcelona anadhani ndani ya miaka miwili au mitatu atakuwa amechukua nafasi ya Messi kama alivyofanya nyota huyo wakati alipokuwepo Ronaldinho. Neymar kwasasa bado ana mkataba na Santos ambao unamalizika baada ya michuano ya Kombe la Dunia 2014.

No comments:

Post a Comment