
Wednesday, April 10, 2013
SASA NIKO FITI - WOODS.
MCHEZA gofu namba moja duniani, Tiger Woods amesema yuko katika kiwango kizuri tayari kukata ukame wa miaka mitano kupita bila kushinda taji kubwa la Masters wiki hii. Woods ndio anapewa nafasi kubwa ya kunyakuwa zawadi ya Koti ya Bluu toka alipofanya hivyo mwaka 2005 na taji la kwanza kubwa toka mwaka 2008 baada ya kurejea kileleni mwa orodha ya wachezaji bora wa mchezo huo kwa kushinda mataji matatu mwaka huu. Nyota huyo alianguka mpaka katika nafasi ya 58 mwaka 2011 kufuatia kukumbwa na kashfa katika maisha yake binafsi na pia kusumbuliwa na majeruhi. Akihojiwa Woods mwenye umri wa miaka 37 amesema kwasasa anajisikia kurejesha makali yake ya zamani hivyo anategemea kufanya vizuri zaidi mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment