
Wednesday, April 10, 2013
MALAGA KUMLALAMIKIA MWAMUZI UEFA.
MKURUGENZI Mtendaji wa klabu ya Malaga, Vicente Casado amethibitisha kuwa klabu hiyo inatarajia kutuma malalamiko yao rasmi Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kuhusu mwamuzi aliyechezesha mpambano wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortumund jana. Katika mchezo huo Malaga walitolewa kwa jumla mabao 3-2 baada ya kwenda sare ya bila ya kufungana katika mchezo wa kwanza uliochezwa Hispania. Mpaka dakika 90 Malaga walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-1 lakini walijikuta wakipoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao mawili ya haraka haraka ambayo yalizua utata mkubwa kwenye mchezo huo. Thomson amesema ni aibu kubwa katika mchezo mkubwa kama huo mwamuzi anakuwa anatoa maamuzi ya ajabu ambayo yanaigharimu timu ushindi wake hivyo hawawezi kulifumbia suala hilo. Ofisa huyi alifika mbali na kudai kuwa wanahisi rais wa UEFA Michel Platini na wengine katika shirikisho hilo walikuwa wakitaka watolewe katika michuano kwani ni rahisi kufanya kitu kama hicho kwa vilabu vidogo kama Malaga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment