
Wednesday, April 10, 2013
LIGI KUU NCHINI UINGEREZA INAHITAJI MABADILIKO - PIQUE.
BEKI wa kati wa klabu ya Barcelona, Gerard Pique amesisitiza kuwa Ligi Kuu nchini Uingereza inatakiwa kufanya mabadiliko kufuatia vilabu vya nchi hiyo kushindwa kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa msimu huu. Kwa mara ya kwanza toka mwaka 1996 hakuna klabu yoyote ya Uingereza iliyopenya katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo huku Manchester United na Arsenal zikikomea katika hatua ya timu 16 bora. Pique amesema wameshazoea Uingereza kuingiza timu tatu katika hatua ya nusu fainali lakini msimu huu wameshindwa kuingiza hata timu moja katika hatua ya robo fainali hiyo ni changamoto kwao kuangalia mahali gani wamejikwaa ili wajirekebishe na kuerejesha heshima yao. Klabu ya Barcelona inakabiliwa na kiraua kigumu leo wakati watakapoikaribisha Paris Saint Germain katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Ufaransa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment