Tuesday, April 9, 2013

HAKUNA DAKIKA ZA MAOMBOLEZO YA THATCHER KWENYE LIGI KUU.

LIGI kuu nchini Uingereza haitarajii kuviambia vilabu nchini humo kutenga dakika moja ya kukaa kimya ili kuomboleza kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Margaret Thatcher katika ratiba zijazo. Thatcher ambaye alikuwa waziri mkuu akitokea chama cha Conservative kuanzia mwaka 1979 mpaka 1990 alifariki dunia jijini London akiwa na miaka 87 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa kipindi kirefu. Mbali na soka lakini pia hakuna dalili zozote za kutenga muda huo wa maombelezo katika mchezo wa kriketi wakati msimu wao mpya wa ligi hiyo utakapoanza kesho. Pia katika mchezo wa jana usiku wa ligi kati ya Manchester United na Manchester City hakuna muda uliotengwa kwa ajili ya tukio hilo kwa madai kwamba soka haihusiani na mambo ya kisiasa. Mbali na Thatcher pia ligi kuu haikutenga muda walipofariki mawaziri wakuu wengine wawili ambao ni James Callaghan na Edward Health, ingawa hata hivyo vilabu vililazimika kutenga muda wa dakika moja baada ya kufariki mama yake Malkia Elizabeth wa pili. 

No comments:

Post a Comment