Tuesday, April 9, 2013

VILABU VYA LIGI KUU MBIONI KUPITISHA MFUMO WA GTL.

CHAMA cha Soka nchini Uingereza kinategemea mfumo wa teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli-GTL kupitishwa na vilabu vya Ligi Kuu nchini humo wiki hii. Wiki iliyopita FIFA iliwazawadia kampuni ya GoalControl ya Ujerumani mkataba wa kufunga mfumo wa GTL katika michuano ya Kombe la Shirikisho itakayofanyika Juni mwaka huu. Vilabu vya Ligi Kuu vitakutana Alhamisi wiki hii huku kukiwa na metegemeo ya kupitisha mfumo wa GTL ili uweze kutumika kwa msimu ujao wakati FA wao wakitaka kufunga mfumo huo katika Uwanja wa Wembley. Katibu Mkuu wa FA, Alex Horne amesema siku zote amekuwa akiukubali mfumo huo uwepo katika soka na mategemeo yake vilabu vya ligi kuu vitapitisha ili uanze kutumika msimu ujao. Kampuni ya Hawk-Eye ya Uingereza ambayo mfumo wake unatumika sana katika michezo ya tenisi na kriketi iko katika mchuano mkali na kampuni zingine tatu zilizopitishwa na FIFA zikiwepo Cairos, GoalControl na GoalRef katika kufukuzia mkataba wa kufunga mfumo huo katika viwanja vya vilabu vya ligi kuu nchini humo.

No comments:

Post a Comment