Tuesday, April 9, 2013

HAKUNA USHAHIDI WA UBAGUZI KWA RIO NA ANTON FERDINAND - FA.

CHAMA cha Soka nchini Uingereza, FA kinajipanga kuliandikia barua Shirikisho la Soka Duniani-FIFA wakidai kuwa hawajapata ushahidi wowote kuonyesha kwamba mashabiki wa Uingereza walifanya vitendo vya kibaguzi kuwalenga ndugu wawili Rio na Anton Ferdinand. Hatua imefikia kufuatia taarifa kuwa kuna nyimbo za kibaguzi zilioimbwa kuwalenga ndugu hao na mashabiki wa nchi yao katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kati ya Uingereza na San Marino. Bodi ya Kupinga mambo ya kibaguzi barani Ulaya ilipeleka malalamiko FIFA kuhusiana na suala hilo lakini FA walikanusha kutokea kwa tukio hilo na kudai hawakupata ushahidi wowote kuhisiana na hilo. Mkurugenzi Mtendaji wa FA Andrian Bevington amesema kuwa walihitajika na FIFA kupeleka taarifa yao mpaka kufikia jana na wamefanya kama walivyoagizwa.

No comments:

Post a Comment