Tuesday, April 9, 2013

UWANJA WA MANE GARRINCHA KUWA TAYARI KUZINDULIWA APRIL 21.

GAVANA wa jiji la Brasilia, Agnelo Queiroz ameahidi Uwanja mpya wa mane Garrincha wenye uwezo wa kubeba mashabiki 71,000 utakuwa tayari kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia likalofanyika nchini humo mwakani. Uwanja huo uliogharimu kiasi cha dola milioni 500 katika ujenzi wake unatarajiwa kuzinduliwa rasmi April 21 mwaka huu na pia utakuwa tayari kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho itakayofanyika June. Baada ya makabidhiano ya uwanj huo kutakuwa na matukio mawili ambapo moja kati ya matukio hayo litafanyika April 18 huku lingine likiwa ni mechi kati ya ufunguzi wa msimu mpya wa ligi ya nchi hiyo kati timu ya Santos na Flamengo April 25. Queiroz amesema mara baada ya michuano ya Kombe la Shirikisho watakuwa na mwaka mwingine mmoja wa kumalizia baadhi ya vitu vidogo vidogo vilivyobakia kwa ajili kuijiandaa rasmi kwa michuano ya Kombe la Dunia. Zaidi ya wafanyakazi 5,000 wameongezwa ili kujaribu kumalizia uwanja huo kwa muda uliopangwa.

No comments:

Post a Comment