
Friday, April 12, 2013
SOKA LA ITALIA LINATAKIWA KUFANYIWA MABADILIKO MAKUBWA.
RAIS wa klabu ya Napoli ya Italia Aurelio De Laurentiis ameungana na kocha wa Juventus Antonio Conte wakitaka kufanyika kwa mabadiliko makubwa katika mfumo wa uendeshaji wa soka la Italia. De Laurentiis ambaye kabla ya kuwa rais wa Napoli alikuwa muongoza filamu, aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa twitter kwa kunahitajika kufanyika mabadiliko katika soka la nchi hiyo ili kuendana na wakati huu iliopo. Wadau wengi wa soka nchini humo wamekuwa wakilalamikia mfumo wa soka la nchi hiyo kwamba ni wa kizamani sana na hauendani na soka la kisasa. Juventus ndio klabu pekee katika Ligi Kuu nchini Italia maarufu kama Serie A kumiliki uwanja wake mwenyewe wakati vilabu vingine vimekuwa vikitumia viwanja vinavyomilikiwa na halmashauri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment