
Friday, April 12, 2013
BAYERM MUNICH YAPATA MAOMBI ZAIDI YA 200,000 YA TIKETI ZA NUSU FAINALI CHAMPIONS LEAGUE.
KLABU ya Bayern Munich ya Ujerumani imedai kuwa imepokea maombi zaidi ya 200,000 ya tiketi kwa ajili ya mechi yao ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya utakaochezwa jijini Munich, huku maelfu ya maombi hayo yakiwa yametolewa kabla ya kufuzu hatua hiyo kwa kuitoa Juventus ya Italia. Ofisa mmoja wa klabu hiyo amesema wamekuwa wakiboresha takwimu zao mara kwa mara na kwasasa wamepata maombi ya tiketi hizo wakati Uwanja wao wa Alianz Arena una uwezo wa kuchukua mashabiki 69,000 pekee. Bayern imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo wakiwa pamoja na wenzao wa Ujerumani Borussia Dortmund na Real Madrid na Barcelona za Hispania. Bayern ambao tayari wametawadhwa kama mabingwa wapya wa Bundesliga huku wakiwa bado wamebakiwa na mechi sita mkononi Jumamosi iliyopita, pia wameshauza tiketi zote za mechi zao zao 17 za nyumbani mwezi mmoja kabla ya kuchezwa kwa mechi hizo za ligi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment