Friday, April 12, 2013

SUAREZ KUCHUNGUZWA NA FIFA.

MSHAMBULIAJI nyota wa Uruguay, Luis Suarez anafanyiwa uchunguzi na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kufuatia tuhuma za kumpiga ngumi beki wa Chile Gonzalo Jara wakati wa mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwezi uliopita. Rais wa Shirikisho la Soka nchini Uruguay-AUF, Sebastian Bauza amethibitisha FIFA kufungua kesi dhidi ya Suarez ambapo amesema mawakili wao wako wanalifanyia suala hilo baada ya FIFA kuwapa mpaka Aprili 17 wawe wamewasilisha utetezi wao. Mwamuzi Nestor Pitana aliyechezesha mchezo huo alishindwa kuona tukio hilo ambapo wachezaji hao walikuwa wakigombea mpira kwenye kona. Taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya Uruguay zimedai kuwa Suarez ambaye anacheza katika klabu ya Liverpool ya Uingereza alikasirika baada ya Jara ambaye pia anacheza Uingereza katika klabu ya ligi daraja la pili ya Nottingham Forest kumkamata sehemu za siri.

No comments:

Post a Comment