
Friday, April 12, 2013
PREMIER LEAGUE KUANZA KUTUMIA MFUMO WA GTL MSIMU UJAO.
LIGI Kuu nchini Uingereza imepiga kura kukubali mfumo wa teknologia ya kompyuta kwenye mstari wa goli-GTL kuanzia msimu wa 2013-2014 na kuipa mkataba kampuni ya Hawk-Eye ya nchi hiyo kufunga mfumo huo. Hawk-Eye au Jicho la Mwewe ni mfumo unaotumia kamera za video saba zinafungwa pembezoni ili kubaini kama mpira umevuka mstari wa goli au la na kudai kuwa ni mfumo ambao una uhakika zaidi wa kufanya kazi kwa asilimia mia moja. Chama cha Soka cha Uingereza kitafunga mfumo huo katika Uwanja wa Wembley kabla ya mchezo wa Ngao ya Hisani utakaofanyika Agosti mwaka huu. Vilabu vikubwa vilipiga kura kukubaliana na mfumo huo wakati wa mkutano wa wenyeviti wa vilabu 20 vya Ligi Kuu nchini humo uliofanyika jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment