Friday, April 12, 2013

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BAYERN VS BARCELONA, DORTMUND VS MADRID.

KLABU ya Bayern Munich ya Ujerumani imepangwa kucheza na Barcelona ya Hispania katika nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Real Madrid wao watakwaana na Borussia Dortmund. Bayern ambao wameshatwaa taji hilo mara tano, watajitupa uwanjani kutafuta nafasi nyingine ya kutwaa taji hilo baada ya kupoteza taji hilo mwaka jana dhidi ya Chelsea ya Uingereza. Kwa upande wa Barcelona ambao wametinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa mara ya sita mfululizo wao watakuwa wakifukuzia taji hilo kwa mara ya tatu ndani misimu mitano. Mechi za kwanza za nusu fainali ya michuano hiyo zinatarajiwa kufanyika Aprili 23 na 24 huku mechi za marudiano zikifanyika Aprili 30 na Mei mosi wakati fainali itapigwa Mei 25 katika Uwanja wa Wembley, Uingereza. 
Kwa upande wa ratiba ya nusu fainali ya Europa League, Chelsea wamepangwa kucheza na FC Basel ya Switzerland wakati Fernerbahce ya Uturuki wao watakwaana na Benfica ya Ureno ambapo mechi za kwanza zitachezwa Aprili 25 na marudiano Mei 2. 

No comments:

Post a Comment