
Saturday, April 6, 2013
UWANJA MWINGINE BRAZIL WAMALIZIKA.
RAIS wa Brazil, Dilma Rousseff amefungua uwanja wa tatu kati ya viwanja 12 ambavyo vitatumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 ambao unauwezo kuchukua watazamaji 50,000 ikiwa ni miezi mitatu zaidi ya muda uliopangwa kumalizika na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Uwanja huo unaoitwa Arena Fonte Nova uliopo kaskazini mwa mji wa Salvador umegharimu kiasi cha dola milioni 296 na utakuwa mojawapo ya viwanja sita vitakavyotumika kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho kuanzia June 15 mpaka 30 mwaka huu. Kuchelewa kwa ujenzi wa viwanja nchini humo kumepelekea FIFA kusogeza mbele muda wa kumalizika mpaka April 15 mwaka huu. Maandalizi ya Kombe la Dunia pamoja na michuano ya Olimpiki 2016 yamekuwa yakienda nyuma ya muda hivyo kuzusha hofu kuhusu uwezo wan chi hiyo kuandaa mashindano hayo makubwa mawili ambayo yatavutia mashabiki wengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment