Saturday, April 6, 2013

MECHI ZA KUFUZU KOMBE LA 2014 HAZIJACHAKACHULIWA - MUTSCHKE.

WACHUNGUZI wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA wanaamini kuwa mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 haijachakachuliwa baada ya mechi zaidi 500 kuchezwa mpaka sasa. Mkuu wa Usalama wa FIFA, Ralf Mutschke aliwaambia waandishi wa habari kuwa mpaka sasa hakuna tetesi zozote walizopata za upangaji wa matokeo na pia wana imani hakuna kitakachotokea mpaka mechi hizo za kufuzu zitakapomalizika. Mechi za kufuzu zipatazo 820 zinatarajiwa kumalizika rasmi Novemba mwaka huu. Kauli hiyo imekuja huku kukiwa kumeundwa kamati maalumu nchini Afrika Kusini kuchunguza tuhuma zinazimkabili rais wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo Kirsten Nematandani za kupanga matokeo ya mechi za Bafana Bafana za kujipima nguvu kabla ya michuano ya Kombe la Dunia 2010.

No comments:

Post a Comment