Saturday, April 6, 2013

SIJALAZIMISHWA KUMPANGA BECKHAM - ANCELOTTI.

MENEJA wa klabu ya Paris Saint-Germain-PSG amekanusha tetesi kuwa alilazimishwa kumchezesha kiungo David Beckham katika mchezo wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona mbao walitoka sare ya mabao 2-2. Katika mchezo huo Ancelotti alichagua kumuanzisha Beckham mwenye umri wa miaka 37 na kumuacha kiungo wa kimataifa wa Italia Marco Verratti. Beckham ambaye ni nahodha wa zamani wa Uingereza ameanzishwa mara moja katika kikosi cha kwanza na mara nyingine nne amekuwa akiingia kama mchezaji wa akiba kabla ya mchezo huo wa Jumatano iliyopita. Ancelotti amesema sio sahihi kusema kwamba mmiliki wa PSG alimwambia ampange Beckham katika kikosi chake kwasababu sio kazi yake na hadhani kama wako wamiliki wa aina hiyo. Kocha huyo amesema katika maisha yake ya ukocha hakuna hata siku moja wamiliki walimlazimisha kuchezesha aina ya wachezaji wanaowataka, sio Silvio Berlusconi wakati yuko AC Milan, Roman Abramovich wakati yuko Chelsea wala bosi wake wa PSG Nasser Al-Khelaifi. Alimuanzisha Beckham katika mchezo huo kwasababu alistahili.

No comments:

Post a Comment