Saturday, April 6, 2013

KOMBE LAZIMA LITUE OLD TRAFORD - FERGUSON.

KOCHA wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson amedai kuwa taji la ubingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza ndio kitu wanachokitilia maanani kwasasa akisisitiza kuwa taji hilo litasaidia kupunguza machungu ya kutolewa katika Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya. United inakabiliwa na mchezo mgumu wa mahasimu wao Manchester City baadae leo wakitegemea kuongeza pengo la alama mpaka kufikia 18 ingawa hatahivyo pengo lililopo hivi sasa litakuwa vigumu kufikiwa. Pamoja na kubakia mechi kadhaa Ferguson alikiri kuwa anaona taji hilo linaelekea Old Traford kwa mara ya 20 katika historia ya klabu hiyo maarufu duniani. Ferguson amesema timu nyingi kama Tottenham Hotspurs, Arsenal, Chelsea, Liverpool na Everton mashabiki wake wamekuwa wakiomba ahata wanyakue taji moja katika msimu hivyo wao kushinda hilo taji moja itakuwa ni ahueni kwa mashabiki wao.

No comments:

Post a Comment