Sunday, April 7, 2013

BEYERN MABINGWA WAPYA WA KIHISTORIA BUNDESLIGA.

KLABU ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani, imefanikiwa kunyakuwa taji lake la 23 la Ligi Kuu nchini Ujerumani kwa kuweka rekodi ya kulichukua mapema zaidi baada ya kushinda mchezo wao wa Jumamosi kwa bao 1-0 dhidi ya Eintracht Frankfurt. Ushindi huo unaifanya Bayern kuweka pengo la alama 20 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote huku wakiwa wamebakiwa na mechi sita mkononi. Bayern imewavua rasmi waliokuwa mabingwa watetezi Borrusia Dortmund baada ya kunyakuwa taji hilo mapema zaidi kuliko klabu yoyote katika miaka 50 ya historia ya ligi hiyo. Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na mchezaji Bastian Schweinsteiger kwa kisigino katika dakika ya 52 na kuisadia timu yake kufikisha alama 75 mbele ya Dortmund ambao wanashika nafasi ya pili abaada ya kuifunga Augsburg kwa mabao 4-2.

No comments:

Post a Comment