Sunday, April 7, 2013

MECHI YA LIGI UAE YAINGIA KWIKWI BAADA YA MWAMUZI WA PEMBENI KUPIGWA.

MECHI ya Ligi ya Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE kati ya timu ya Al Ain na Al Ahli ilibidi imalizike mapema jana baada ya mwamuzi wa pembeni kupigwa na kitu mfano wa chuma na kumuacha akimwagika damu. Mwamuzi wa kati alilazimika kusimamisha pambano lililokuwa likielekea dakika za mwisho baada ya mwenzake kuumizwa na mashabiki wa timu ya Al Ahli ambao walikuwa na hasira baada ya mwamuzi kukataa kuwapa penati. Pambano lililomalika kwa sare ya bila ya kufungana limeifanya Al Ain kujikita kileleni wakiwa na alama 50 mbele ya Al Ahli ambao wanatofautiana kwa alama 10, ingawa hata hivyo wasimamizi wa ligi hiyo wamesema matokeo hayo yatasimamishwa mpaka uchunguzi utakapomalizika. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao imedai kuwa matokeo ya mechi hiyo yatasimamishwa mpaka uamuzi kutoka kamati ya nidhamu utakapotolewa kutokana na tukio hilo lililomuhusisha mwamuzi.

No comments:

Post a Comment