Sunday, April 7, 2013

NI MESSI PEKEE ANAYEWEZA KUFUNGA MABAO 50 KWA MSIMU - ALLEGRI.

MENEJA wa klabu ya AC Milan ya Italia, Massimiliano Allegri amempoza mshambuliaji wake Stephen El Shaarawy pamoja na ukame wa mabao alionao toka kuanza kwa mwaka huu. El Shaarawy mwenye umri wa miaka 20 alikuwa akiongoza kwa kufunga mabao kabla ya msimu haujafikia katikati lakini baada ya hapo amekuwa na ukame wa mabao baada ya kufunga mabao mawili katika mechi 13 alizocheza. Pamoja na kushindwa kufunga mabao Allegri anaamini kuwa kinda huyo anaweza kurejea tena katika makali yake baadae kwasababu ni kawaida kwa mshambuliaji kukutwa na hali hiyo baada ya msimu mrefu. 
Allegri amesema katika maisha yake anamfahamu mchezaji mmoja ambaye anaweza kufunga mabao 40 mpaka 50 kwa msimu mmoja na mchezaji huyo anacheza katika klabu ya Barcelona, akimtolea mfano Lionel Messi.

No comments:

Post a Comment