Tuesday, May 14, 2013

AUBAMEYANG ANYAKUWA TUZO YA MARC-VIVIEN FOE 2013.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Gabon, Pierre-Emirick Aubameyang ametajwa kunyakuwa tuzo ya Marc-Vivien Foe kwa mwaka huu nchini Ufaransa baada ya kuwashinda nyota wa Cameroon Nicolas Nkoulou na Jonathan Pitroipa wa Burkina Faso. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 anayecheza katika klabu ya Saint Etienne alipata alama 209 mbele ya Nkoulou anayecheza klabu ya Olympique Marseille aliyepata alama 81 wakati mchezaji bora wa mashindano ya Mataifa ya Afrika 2013 Pitroipa alipata alama 35. Waandishi wa habari wa habari za michezo wapatao 68 walishiriki zoezi hilo la upigaji kura na kumpa ushindi mshambuliaji huyo ambaye anashika nafasi ya pili kwa ufungaji katika Ligi Kuu nchini Ufaransa. Tuzo hiyo ambayo hutolewa kwa mshindi mara moja pekee mwaka jana ilikuwa ikishikiliwa na mshambuliaji wa Morocco Younes Belhanda.

No comments:

Post a Comment