Tuesday, May 14, 2013
WILSHERE KUIKOSA BRAZIL MWEZI UJAO.
KIUNGO nyota wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Arsenal anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo wa kifundo cha mguu mwishoni mwa msimu hatua ambayo itamkosesha michezo ya kirafiki wa kimataifa baina ya nchi yake dhidi ya nchi za Ireland ya Kaskazini na Brazil. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 anatarajiwa kuanzia katika benchi la wachezaji wa akiba katika mechi ya nne mfululizo ya Ligi Kuu nchini Uingereza wakati Arsenal watapowakaribisha mabingwa wapya wa Kombe la FA Wigan Athletic baadae leo. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kiungo huyo kwasasa anacheza huku akitumia dawa za kutuliza maumivu na atamtumia wakati ambao atahitajika sana ndio ameona ni vyema nyota huyo akafanyiwa upasuaji mdogo ili kutibu tatizo lake la kifundo cha mguu. Wilshere ambaye ambaye amecheza mechi saba akiwa na timu ya taifa ya Uingereza, alikosa msimu wa mwaka 2011-2012 kutokana na matatizo ya kifundi cha mguu na kisigino na pia alikaa nje kwa wiki kadhaa baada ya kupata tena tatizo la kifundo cha mguu Machi mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment