Tuesday, May 14, 2013
ROMA WALIMWA FAINI KWA UBAGUZI.
KLABU ya AS Roma ya Italia imetozwa faini ya euro 50,000 kwa tabia ya kibaguzi iliyoonyeshwa na mashabiki wake katika mchezo wa Serie A dhidi ya AC Milan Jumapili iliyopita mpaka kupelekea mwamuzi wa mchezo huo kusimamisha pambano kwa muda. Kamati ya nidhamu ya ligi hiyo iliyokutana ilidai kuwa imewakuta na hatia mashabiki wa Roma kwa kupiga kelele za kibaguzi kuwaendea wachezaji watatu wa Milan ambao ni weusi. Mchezo huo ulisimamishwa kwa dakika mbili mwanzoni mwa kipindi cha pili kupisha matangazo ya kuwakataza mashabiki hao kuendelea kufanya vitendo hivyo na baada ya kutulia mchezo uliendelea kama kawaida. Pamoja na kwamba kamati hiyo haikutana ni wachezaji gani waliokuwa walengwa katika tukio hilo lakini kocha wa Milan Massimiliano Allegri amesema mashabiki hao walimlenga Mario Balotelli. Katika mchezo huo Milan iliwacheza wachezaji watano weusi katika kikosi kilichoanza ingawa hata hivyo Sulley Muntari alitolewa kabla ya mapumziko kwenye mchezo huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment