Tuesday, May 14, 2013
HATIMAYE MANCINI KIMEOTA.
KLABU ya Manchester City hatimaye imemtimua kocha wake Roberto Mancini ikiwa ni mwaka mmoja umepita toka kocha huyo aisaidie timu hiyo kunyakuwa taji lake la kwanza la Ligi Kuu nchini Uingereza. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika mtandao wa klabu hiyo ilithibitisha kusitisha mkataba na kocha huyo kwasababu ya kushindwa kufikia mojawapo ya malengo waliyojiwekea msimu huu. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa kocha msaidizi Brian Kidd ndiye atakayepewa mikoba kwa ajili ya mechi mbili za ligi zilizobakia pamoja na ziara yao ya Marekani wakati mchakato wa kutafuta kocha mpya ukiendelea. Kumekuwa na tetesi kuwa kocha wa klabu ya Malaga ya Hispania Manuel Pellegrini ndio anayepewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Mancini lakini mwenyewe alikanusha tetesi hizo akidai kuwa hakuna lolote lililoafikiwa juu ya yeye kwenda City.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment