Thursday, May 23, 2013
BERLIN KUWA MWENYEJI WA FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE 2015.
SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya, UEFA limesema kuwa mji wa Berlin utakuwa mwenyeji wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza mwaka 2015 na jiji la Warsawa nchini Poland litakuwa mwenyeji wa michuano ya Europa League. Uwanja wa Olimpiki wa Berlin kwa mara ya kwanza utakuwa mwenyeji wa fainali hiyo katika mji mkuu huo wa Ujerumani ambao ulikuwa mwenyeji wa michuano ya olimpiki mwaka 1936 na mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2006. Hatua hiyo imekuja kwa wakati baada ya timu mbili za nchi hiyo Bayern Munich na Borussia Dortmund kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mchezo ambao unatarajiwa kupigwa Jumamosi katika Uwanja wa Wembley, jijini London Uingereza. Rais wa Shirikisho la Soka la Ujerumani-DFB, Wolfgang Niersbach amesema katika taarifa yake kwa walikuwa wameweka nia kwa rais wa UEFA Michel Platini katika fainali ya Munich mwaka jana kwamba wangependa kuandaa tena fainali hiyo mapema hivyo anashukuru ombi lao limekubaliwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment