Friday, May 24, 2013

MALI WAPELEKA MALALAMIKO FIFA KUHUSU SUALA LA KOCHA WAO KUSAINI MKATABA NA MAZEMBE.

RAIS wa Shirikisho la Soka nchini Mali-MFF, Hammadoun Kola Cisse amepeleka malalamiko Shirikisho la Soka-FIFA baada ya kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya TP Mazembe ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC mapema wiki hii. Cisse amesema kitendo cha Carteron raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 42 kusaini mkataba na Mazembe kimekiuka kanuni za mkataba wake ambao unamalizika Juni 30 mwaka 2014. Kiongozi aliendelea kusema kuwa wameshangazwa na kitendo kilichofanywa na kocha huyo kwani walikuwa hawana taarifa zozote kuhusiana na suala hilo ndio maana wameamua kulipeleka FIFA ili waweze kutoa maamuzi. Kocha huyo alitakiwa kuiongoza mali katika mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Rwanda Juni 9 na Benin Juni 16, ingawa hata hivyo viongozi wamesema kocha msaidizi Amadou Pathe Diallo atachukua mikoba ya Carteron kwa muda.

No comments:

Post a Comment