Saturday, May 11, 2013

BOATENG, ESSIEN, AYEW BADO SANA KUREJEA BLACK STARS - KONADU.

KOCHA msaidizi wa timu ya taifa ya Ghana, Maxwell Konadu amesema kuwa wachezaji nyota wa nchi hiyo Kevin-Prince Boateng, Michael Essien na Andre Ayew hawatarejea katika timu hiyo mapema. Boateng aliamua kuacha kuichezea timu ya taifa mwaka 2011 na kumekuwa na tetesi kuwa anataka kurejea wakati Essien na Ayew wao pia waliomba muda wa kupumzika ili wazitumikie klabu zao vyema. Konadu amebainisha kuwa hana uhakika wa lini nyota hao wataamua kurejea katika timu ya taifa na kudai kuwa hata kama hilo litatokea haitakuwa katika siku za karibuni. Kuhusu Boateng, Konadu amesema habari za kurejea hata yeye anazisikia lakini hazijamfikia rasmi na kocha mkuu Kwesi Appiah hajamwambia lolote kuhusiana na suala hilo. Ghana inatarajiwa kupambana na Sudan na Lesotho mwezi ujao katika mechi za kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2014.

No comments:

Post a Comment