
Saturday, May 11, 2013
ROONEY AVISHANGAA VYOMBO VYA HABARI.
MSHAMBULIAJI nyota wa Manchester United Wayne Rooney amejibu madai kwamba ameondoa jina la timu hiyo katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa twitter ikiwa ni kama sehemu ya kuishiniza klabu hiyo kumuuza. Nyota huyo aliripotiwa kumwambia bosi wake Sir Alex Ferguson wiki mbili zilizopita kuwa anahitaji kuondoka Old Traford baada ya kushindwa kuvumilia kukaa benchi katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu nchini Uingereza. Hatahivyo Ferguson aliripotiwa kukataa ombi la nyota huyo na kudai kuwa hawana mpango wa kumuuza. Nyota huyo mara baada ya kusikia habari hizo alijitetea akidai kuwa hazina maana yoyote kwani hajui habari hiyo magazeti huwa wanazitoa wapi kwani twitter yake haikuwa na jina hilo toka zamani. Rooney amesema kilichotokea aliombwa na kampuni ya Nike kuongeza jina la kampuni hiyo katika twitter yake kama wadhamini wengine wanavyofanya lakini cha kushangaza hakuna aliyeandika hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment