
Saturday, May 11, 2013
VUVUZELA LA BRAZIL LAZUA TAFRANI.
POLISI wa kaskazini-mashariki nchini Brazil wamefungia vifaa mfano wa vuvuzela kutumika katika viwanja vya soka katika eneo hilo kwasababu za kiusalama. Vifaa hivyo ambavyo vinaitwa Caxirola, havitaruhusiwa katika Uwanja wa Fonte Nova mwishoni mwa wiki hii kwasababu ya mashabiki walioshindwa kudhibiti hasira zao baada ya timu yao kufungwa mwezi uliopita na kuanza kurusha vifaa hivyo uwanjani na kuleta taharuki kwa muda. Vifaa hivyo ambavyo vimepitishwa rasmi na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kutumika katika michuano ya Kombe la Dunia 2014, pia vitatumika wakati wa michuano ya Kombe la Shirikisho itakayoanza kutimua vumbi mwezi ujao. Caxirola ni vifaa vilivyotengezwa kwa plastiki na hutoa mlio laini kuliko ule wa vuvuzela ambazo zilitumika katika michuano ya Kombe la Dunia 2010 iliyofanyika nchini Afrika Kusini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment