Saturday, May 11, 2013

UNITED WALINIPA OFA AMBAYO NILISHINDWA KUKATAA - MOYES.

Kocha wa klabu ya Everton David Moyes ambaye msimu ujao atahamia klabu ya Manchester United, amesema hakupanga kuondoka Goodison Park ila ilikuwa vigumu kukataa ofa ya kuifundisha United. Moyes mwenye umri wa miaka 50 ameyasema hayo wakati akizungumzia mchezo wa siku ya jumapili wa ligi kuu soka nchini England. Kauli hiyo ameitoa siku moja baada ya kutangaza rasmi ataicha Everton mwishoni mwa msimu huu na kujiunga na United kama mrithi wa Sir Alex Ferguson ambaye alitangaza kustaafu kufundisha soka baada ya msimu huu kumalizika. Kocha huyo raia wa Scotland amesema kuwa alipanga kuongeza muda wa kuifundisha Everton baada ya kukaa kwa miaka 11, lakini alipopewa mkataba wa miaka sita wa kuifundisha United alishindwa kukataa.

No comments:

Post a Comment