SHIRIKISHO la Soka barani Afrika-CAF limetangaza kumfungia rais wa Shirikisho la Soka la Liberia kwa kipiindi cha miezi sita. Uamuzi huo umefikiwa mara baada ya mkutano wa bodi ya nidhamu ya CAF uliofanyika jijini Marrakech, Morocco. Rais huyo Musa Bility alikutwa na hatia kwa kukiuka katiba ibara ya pili na saba kwa kutumia taarifa ya kikao cha kamati ya utendaji ya CAF bila idhini ya shirikisho hilo. Kifungo hicho kitamzuia Bility kujishughulisha na masuala yoyote ya soka kwa kipindi cha miezi sita huku shirikisho la soka la nchi yake likitakiwa kulipa kiasi faini ya dola 10,000.
No comments:
Post a Comment