Friday, May 3, 2013

MICHUANO YA COSAFA YAIVA.

BARAZA Michezo kwa nchi za Kusini mwa Afrika-COSAFA limetangaza miji ambayo michuano inayoandaliwa na baraza itachezwa nchini Zambia kuanzia Julai 6 mpaka 21 mwaka huu. Katika taarifa yake iliyotumwa kwa vyombo vya habari COSAFA wamesema michuano hiyo itachezwa katika miji ya Lusaka ambao ni mji mkuu wa Zambia, Ndola, Kabwe na Kitwe. Michuano hiyo mwaka huu ambayo itashirikisha nchini za Afrika Mashariki na Kati, Kenya na Tanzania pia kutakuwa na nchi za Botswana, Namibia, Lesotho, Swaziland, Mauritius na Seyshelles katika hatua za makundi. Zingine zitakuwa wenyeji Zambia, Afrika Kusini, Angola, Zimbabwe, Msumbiji na Malawi, huku ratiba kamili ikitarajiwa kupangwa katika hoteli ya Southern Sun Ridgeway jijini Lusaka baadae leo.

No comments:

Post a Comment