MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Inter Milan, Antonio Cassano anatarajiwa kukosa mechi ya mwisho ya Ligi Kuu nchini Italia dhidi ya Udinese baada ya kuvunjika mkono wakati wa mazoezi. Taarifa iliyotolewa katika mtandao wa klabu hiyo imedai kuwa nyota huyo aliangukia mkono wake wakati wa mazoezi na baada ya kufanyiwa vipimo iligundulika kuwa umevunjika hivyo hataweza kumalizia mechi ya mwisho msimu huu. Cassano ambaye amefunga mabao saba katika ligi msimu huu, ndio alikuwa amerejea baada kukaa nje kwa mwezi mmoja akiuguza majeraha ya msuli. Inter kwasasa inashika nafasi ya tisa katika ligi wakiwa na alama 54 na hawatashiriki michuano ya Ulaya msimu ujao baada ya kampeni zao kushindwa kutokana na wachezaji wengi nyota kuwa majeruhi akiwemo Diego Milito, Rodrigo Palacio na Dejan Stankovic.
Friday, May 17, 2013
CASSANO AVUNJIKA MKONO.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment