Saturday, May 18, 2013
DUNIA NZIMA INANIHITAJI - HEYNCKES
MENEJA wa klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani, Jupp Heynckes amedai kuwa dunia nzima imewasiliana nae kumtaka kuendelea na kazi ya ukocha mara baada ya kumalizika kwa mkataba wake na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu. Heynckes mwenye umri wa miaka 68 atampisha kocha mpya Pep Guardiola baada ya kuinoa klabu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili na kuiwezesha kunyakuwa taji la Ligi Kuu nchini Ujerumani, Bundesliga msimu huu na kufika fainali kwa mara ya tatu mfululizo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwa mafanikio hayo Heynckes amesema tayari vilabu mbalimbali tayari vimefanya naye mazungumza kufuatia Bayern kutangaza Januari kuwa kocha huyo ataondoka mwishoni mwa msimu lakini amesisitiza kuwa bado anasubiri aone ataelekea wapi. Kocha huyo amesema kwasasa fikra zake zote ziko mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund kwani bado hajamaliza mkataba wake rasmi na Bayern.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment