Saturday, May 18, 2013
BRAZIL YANUNUA ROBOTI KUIMARISHA USALAMA.
SERIKALI ya Brazil imesema baadhi ya roboti za kuimarisha usalama zilizonunuliwa kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia 2014 zitakuwa tayari kutumika wakati wa Kombe Shirikisho itakayoanza kutimua vumbi Juni mwaka huu. Kampuni ya iRobot imesema roboti 30 zitawasilishwa kabla ya mwisho wa mwaka pamoja na vipuri na vifaa vingine vya kusaidia katika kuzitumia. Serikali ilithibitisha Alhamisi kuwa baadhi zitakuwa tayari kutumiwa katika miji sita itakayokuwa wenyeji wa mechi za Kombe la Shirikisho. Kampuni hiyo imesema serikali ya Brazil iliyotia saini mkataba wa $7.2 milioni, ambao unahusisha magari madogo yasiyokuwa na dereva ambayo yanaweza kutumiwa kupeleleza, kupekua na kuondoa mabomu pamoja na shughuli nyingine za kudumisha utawala wa sheria. Michuano ya Kombe la Shirikisho ni ya kwanza katika msururu wa hafla za ngazi ya juu za michezo zitakazoandaliwa na Brazil, ikiwa ni pamoja na Kombe la Dunia na Olimpiki 2016 jijini Rio de Janeiro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment