Saturday, May 18, 2013

MASHABIKI BAYERN WAGOMBEA TIKETI ZA KUTIZAMA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA KATIKA LUNINGA YA ALLIANZ ARENA.

MASHABIKI wa klabu ya Bayern Munich wamelazimika kukaa kwenye foleni zaidi ya saa 12 na kununua tiketi zote 45,000 za kuangalia mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund katika luninga kubwa kwenye Uwanja wa Allianz Arena mchezo ambao utakaochezwa utachewa jijini London Mei 25 mwaka huu. Tiketi zote kwa ajili ya mchezo huo wa fainali hiyo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Wembley na kushirikisha timu zote za Ujerumani ziliuzwa ndani ya muda saa sita pekee toka ziingie sokoni. Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imedai kuwa mara baada ya tangazo la kuuzwa kwa tiketi hizo kutoka mashabiki walianza kupanga foleni kuanzia usiku wa nne foleni ambayo ilifikia urefu wa mpaka mita 400 na saa sita baadae tiketi zote zilimalizika. Bayern ambao wamenyakuwa taji lao la 23 la Bundesliga wiki chache zilizopita, kwasasa wanafukuzia kushinda mataji matatu ndani ya msimu mmoja kufuatia fainali nyingine ya Kombe la Ujerumani dhidi ya VfB Stuttgart watakayocheza Juni mosi.

No comments:

Post a Comment