Wednesday, May 8, 2013

DIOUF KUTIMKIA GUINEA MWISHONI MWA MSIMU.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Senegal, El Hadji Diouf anatarajiwa kujiunga na klabu ya AS Kaloum ya Guinea wakati wa kipindi cha usajili kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na rais wa klabu hiyo Boubah Sampil. Diouf mwenye umri wa miaka 32ambaye amewahi kucheza katika klabu za Liverpool na Sunderland kabla ya kuhamia Leeds United ambayo iko katika daraja la pili nchini Uingereza anatarajiwa kupewa mkataba wa miaka minne katika timu hiyo yenye maskani yake jijini Conakry. Akiwa huko Diouf atakutana na Amara Traore ambaye ameteuliwa kuwa kocha wa Kaloum baada ya kutimuliwa kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Senegal mwaka uliopita. Hii itakuwa mara ya kwanza kwa nyota huyo ambaye amewahi kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mara mbili kuchezwa soka la kulipwa katika bara la Afrika.

No comments:

Post a Comment