Wednesday, May 8, 2013

KIPA WA IVORY COAST ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI.

GOLIKIPA wa kimataifa wa Ivory Coast, Copa Barry ameruhusiwa kutoka hospitali nchini Ubelgiji jana baada ya kukimbizwa hospitali kutoka uwanja wakati wa mechi ya ligi baina timu yake ya Lokeren na FC Bruges. Barry mwenye umri wa miaka 33 alijigonga kwenye mojawapo ya nguzo langoni mwake wakati akijaribu kuokoa mpira na kuzimia kwa dakika kadhaa kabla ya kukimbizwa hospitali ya karibu. 
Taarifa ya matibabu yake imedai kuwa Barry alisumbuliwa na mtikisiko mwepesi wa ubongo lakini anaendelea vyema hata hivyo atakaa nje ya uwanja kwa wiki moja zaidi. Barry ni golikipa chaguo la kwanza la timu ya taifa ya Ivory Coast na habari za kuzimia kwake zilizua hofu mwishoni mwa wiki iliyopita katika nchi hiyo iliyopo magharibi mwa Afrika, haswa ikizingatiwa kuwa wanajiandaa kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Gambia.

No comments:

Post a Comment