Tuesday, May 21, 2013
FERGUSON ALAMBA TUZO YA MENEJA BORA WA MWAKA.
CHAMA cha Makocha wa Ligi Kuu nchini Uingereza kimemteua Aliyekuwa meneja wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson kuwa meneja bora wa mwaka wa ligi hiyo. Ferguson ambaye amestaafu mwishoni mwa msimu huu baada ya kuifundisha United kwa kipindi chamiaka 26 anakuwa kocha wa kwanza kushinda tuzo hiyo mara nyingi zaidi ambayo hupigiwa kura na makocha wenzake. Akipokea tuzo yake kutoka kwa meneja wa West Ham United Sam Allardyce katika sherehe hizo jana usiku, Ferguson alitania kuwa mmiliki wa West Ham Steve Clarke anatakiwa naye apewe tuzo kwa timu yake kuifunga United mabao matano katika mchezo baina ya timu hizo uliochezwa Jumapili. Ferguson amesema sare ya mabao 5-5 waliyopata dhidi ya West ham kila atakuwa akiikumbuka kwa kipindi kirefu kijacho na kwa upande mwingine anashukuru amemaliza kazi hiyo ya ukocha kwasababu ni moja ya shughuli ngumu kabisa duniani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment