Thursday, May 9, 2013

FERGUSON KUAGWA RASMI JUMAPILI.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson anatarajiwa kukaa kwa mara ya mwisho katika benchi la ufundi la Old Traford mwishoni mwa wiki wakati timu hiyo itakapoikaribisha Swansea City, baada ya kutangaza kustaafu mwishoni mwa msimu. Katika mchezo huo ambao badala ya kuwa wa furaha utakuwa na huzuni kidogo wakati kocha huyo akiaga, United itakabidhiwa rasmi Kombe la Ligi Kuu nchini Uingereza walilotwaa msimu huu. Ferguson mwenye umri wa miaka 71 ameiongoza United kwa kipindi cha miaka 26 na kuisaidia kutwaa mataji mengi yakiwemo 13 ya ligi, mawili ya ligi ya mabingwa Ulaya, matano ya FA na manne ya Kombe la Ligi. Mashabiki ambao watakosa tiketi za kwenda kushuhudia mechi hiyo ya mwisho kwa Ferguson Old Traford watapata nafasi siku ya Jumatatu ijayo kushikana mkono na kumuaga wakati timu hiyo itakapofanya matembezi katika mitaa ya jiji la Manchester kutembeza kombe lao. United imepanga kutangaza mrithi wa Ferguson katika kipindi kifupi kijacho huku kocha wa Everton akipewa nafasi kubwa ya kuionoa klabu hiyo akifuatiwa na kocha wa Real Madrid Jose Mourinho.

No comments:

Post a Comment