Thursday, May 9, 2013

RONALDO AFUNGA BAO LA 200.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo amefanikiwa kufunga bao lake la 200 akiwa na klabu hiyo katika ushindi wa mabao 6-2 waliopata dhidi ya Malaga kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania, La Liga. Pamoja na kushuhudia penati yake aliyopiga ikiokolewa na golikipa Willy Caballero dakika ya 22 lakini nyota huyo hakuta tama baada ya kufunga bao dakika chache baadae akimalizia pasi fupi ya Xabi Alonso na kutengeneza mabao mengine ambayo yalifungwa na Mesut Ozil na Karim Benzema. Ronaldo amefikisha idadi hio ya mabao kwa mechi 197 alizocheza Madrid na sasa amefikisha mabao 54 katika mechi 53 alizocheza msimu huu katika ngazi ya klabu. Akiwa na mabao hayo 200 Ronaldo amekwea mpaka nafasi ya sita katika wafungaji hodari waliowahi kucheza Madrid, akiwa nyuma ya mabao nane ya nguli wa Mexico Hugo Sanchez anayeshika nafasi ya tano katika orodha hiyo.

No comments:

Post a Comment