Tuesday, May 14, 2013

MESSI KUKAA NJE WIKI TATU.

KLABU ya Barcelona imepokea habari za kuhuzunisha kutoka upande wa kitabibu baada ya kuarifiwa na madaktari wa timu hiyo kwamba watakosa huduma ya mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Lionel Messi kwa kipindi cha wiki mbili mpaka tatu kutokana na matatizo ya msuli yanayomsumbua. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina alipata maumivu ya msuli wa paja wakati wa mchezo baina ya timu yake na Atletico Madrid mwishoni mwa wiki iliyopita na kupelekea kutolewa katikati ya kipindi cha pili. Messi alifanyiwa vipimo zaidi leo ili kujua ukubwa wa tatizo na kuthibitisha kuwa nyota huyo atakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha kati ya mbili au tatu. Nyota huyo mwenye umri wamiaka 25 atakosa mechi za La Liga dhidi ya Valladolid na Espanyol huku pia kukiwa na uwezekano wa kukosa mechi ya mwisho dhidi ya Malaga Juni 1 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment