Tuesday, May 14, 2013
NEYMAR ATAKWENDA BAYERN MUNICH - CASCIONE.
OFISA wa zamani wa klabu ya Santos ya Brazil, Vicente Cascione amedai kuwa mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Neymar ataondoka kwenda klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani katika kipindi cha majira ya kiangazi kuungana na kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola. Barcelona ndio wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kupata saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye amepanga kwenda Catalunya baada ya michuano ya Kombe la Shirikisho kuzungumzia uhamisho wake wakati Real Madrid nao wakimnyatia kimya kimya nyendo zake. Hata hivyo, Cascione amesisitiza kuwa Neymar atakwenda kucheza katika Ligi Kuu nchini Ujerumani, Bundesliga kwani tayari taratibu za uhamisho kwenda Allianz Arena umeshakamilika. Ofisa huyo aliandika katika blog yake kuwa amezinasa taarifa hizo akiwa wa kwanza kwamba Neymar tayari ameshamwaga wino Bayern hivyo hatakwenda Hispania kama inavyodhaniwa na wengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment